JUHUDI ZA UONGOZI WA YANGA KUMSHAWISHI JUMA MAGOMA KUFUTA KESI ZAKWAMA

JUHUDI za uongozi wa Yanga kumaliza mivutano na baadhi ya wanachama wake ili kurudisha mshikamano na umoja, zimeshindwa kuzaa matunda.

Hivi majuzi, uongozi wa timu hiyo chini ya Makamu Mwenyekiti wake, Clement Sanga, ulizungumza na baadhi ya watu akiwemo Juma Magoma aliyefungua kesi mahakamani kupinga klabu hiyo kukodishwa.

Sanga alimwita Magoma pamoja na watu wengine wakiwemo wazee wa klabu hiyo wakiongozwa na katibu wa baraza la wazee, Ibrahim Akilimali.


Hata hivyo, mazungumzo hayo yaliyofanyika makao makuu ya klabu hiyo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, jijini Dar es Salaam hayakuzaa matunda kutokana na Magoma na washirika wake kukataa kuifuta kesi hiyo.

No comments