KALALA JR WA TWANGA ANUSURIKA KUFA KWA AJALI MBAYA YA GARI


Mwimbaji tegemeo wa Twanga Pepeta, Kalala Jr jana usiku alipata ajali mbaya ya gari wakati akiwa njiani kurejea Dar es Salaam akitokea Dodoma.

Kalala alikuwa kwenye gari Toyota Harrier ya mbunge wa Nyamagana Mh. Mabula ambapo ikiwa na watu watano ndani yake ikapata ajali mbaya maeneo ya Mvumero majira ya saa 3 usiku.

Mwimbaji huyo na mheshimiwa Mbunge walipata maumivu madogo lakini watu wengine wawili waliumia vibaya.

Wote akiwemo Kalala walikimbizwa hospitali ya mkoa wa Morogoro na kupata matibabu.

Akiongea na Saluti5 kutoka hospitalini hapo asubuhi hii, Kalala Jr akasema chanzo cha ajali ni trekta iliyoingia barabarani ghafla bila viashiria vyoyote.

“Tuligonga trekta ambayo haikuwa na taa zozote na gari yetu ikapinduka na kuharibika vibaya sana,” alisema Kalala ambaye amefafanua kuwa ana maumivu ya mkono na kifua.

Kalala alikuwa na bendi yake ya Twanga Pepeta ndani ya Dodoma ambapo ilifanya maonyesho mawili Jumamosi na Jumapili.
 Toyota Harrier ikiwa imeharibika vibaya baada ya ajali
 Mmoja wa watu walioumia sana
Kalala alipokuwa kifanyiwa vipimo vya kifua

No comments