Habari

KAMA ULIKUWA HUJUI… KIBAO “SIWALAUMU WAKWE” CHA MLIMANI PARK SIKINDE NI “DONGO” KWA REHEMA TAJIRI NA BABA YAKE MZEE JANJA

on

SIRI ya kuwa kibao “Siwalaumu
Wakwe” cha Mlimani Park Sikinde ni tukio la kweli, imefichuka hivi karibuni
baada ya mwimbaji mahiri Rehema Tajiri kuhojiwa na mtangazaji Rajab Zomboko wa
kipindi cha Afro Tz na kuweka bayana kila kitu.

Kwenye moja ya mfululizo wa
kipindi hicho kinachorushwa na Radio One, Rehema alisema hivi karibuni kuwa
kibao hicho kilitungwa na Max Bushoke aliyekuwa mpenzi wake kwa wakati huo,
baada ya kukataliwa barua ya posa na baba mkwe wake, marehemu Hamis Tajiri.
Rehema alisema kuwa, mzee Tajiri
alikataa Bushoke asimuoe kwasababu ya tofauti ya dini zao, sifa mbaya ya kabila
la Max la Kihaya kwa wakati ule, ukorofi pamoja na ulevi wa kupindukia aliokuwa
nao.
“Nakumbuka Max alikitunga kibao
hicho kule kwenye jumba lao la DDC ya Mlimani tukiwa tumekaa na nikiwa sina
hili wala lile, tena huku akiniambia kuwa anaamua kumweleza ukweli baba yangu,”
alisema rehema.
Alisema kuwa, awali alifikiri Max
anatania lakini alikuja kubaini kwamba alikuwa ameamua baada ya siku nyingine
baadae kuingia kwenye dansi la Sikinde DDC Kariakoo na kusikia kibao hicho
kikitambulishwa kwa mashabiki.

Rehema alisema kuwa, baada ya
kibao hicho kurekodiwa na kuanza kusikika radioni, mzee Tajiri aligundua kwamba
amepigwa “dongo” na Max lakini aliishia kumwambia bintie tu kuwa anaelewa kila
kitu kuhusu wimbo huo.


Usikilize hapo juu wimbo huo.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *