KAMATI YA NIDHAMU TFF YAWAITA “KIKAANGONI” WANAFAMILIA WA CHAMA CHA SOKA RUKWA


KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF), imeagiza sekretarieti yake kuwaita tena wanafamilia watatu wa Chama cha soka Rukwa (RUREFA).

Wajumbe hao walioshitakiwa mbele ya kamati hiyo ya nidhamu ni mwenyekiti wa RUREFA, Blassy Kiondo, Mwenyekiti wqa Kamati ya Uchaguzi, James Makwinya na Kaimu Katibu Mkuu wa chama hicho, Ayoub Nyaulingo.

Madai dhidi ya wanafamilia hao wa moira wa miguu ni kudharau maagizo ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF ya kuwataka kusimamisha mchakato wa uchaguzi wa mkoa mpaka rufaa zilizowasilishwa TFF zitakaposikilizwa.

TFF ilipeleka mwito wa kuwataka washitakiwa hao kwenda mbele ya Kamati ya Nidhamu Machi 8, mwaka huu lakini wote hawakutokea kwa sababu mbalimbali.


Kwa kuzingatia kanuni za nidhamu, Kamati imeona ni vyema watuhumiwa wakapata nafasi ya kwenda kujitetea mbele ya kamati hiyo na kwamba ikitokea wameshindwa kufika, watume wawakilishi au wajitetee kwa njia ya maandishi katika kikao kingine kitakachofanyika Machi 15, mwaka huu saa 12:00 jioni.

No comments