"KIBERENGE" CHA DRC KONGO NJE WIKI SITA KWA JERAHA LA GOTI

KULE nyumbani kwao Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wanamwita "Kiberenge" kutokana na uwezo wa nguvu zake nyingi uwanjani.

Huyu pia ni mshambuliaji wa Klabu ya Hull City, Dieumerci Mbokani ambaye katika fainali za michuano ya mataifa ya Afrika nnchini Gabon (AFCON) alikuwa mwiba kwa kila timu ambayo walikumbana nayo.

Lakini sasa habari mbaya ni kwamba mchezaji huyo hatocheza kwa kipindi cha wiki sita baada ya kupata jeraha la paja.

Mshambuliaji huyo wa DRC Congo mwenye umri wa miaka 31, ambaye yuko kwa mkopo katika Klabu ya Dynamo Kiev, alibadilishwa wakati wa sare ya 1-1 dhidi ya Burnley.

"Ni pengo kubwa kwetu kumkosa Mbokani. Amekua msaada mkubwa kutokana na uwezo wake na kwa jinsi anavyopambana uwanjani,”amelalama kocha wa timu hiyo, Marco Silva.

Kocha huyo amesema kwamba ni kawaida kwa mchezaji kuumia, lakini akasema kuwa kuumia kwa Kiberenge hicho kunawapa wakati mgumu katika mechi zinazoendelea.

“Tutakuwa katika wakati mgumu lakini ngoja tukubali kwamba kuumia kwa mchezaji ni sehemu ya kuendesha soka,” amesema.

Hull pia imethibitisha kuwa jeraha la goti alilopata beki Harry Maguire wakati wa mechi dhidi ya Burnley sio baya sana kama ilivyodhaniwa.


Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 anatarajiwa hata hivyo kwamba huwenda angepona na kuwa tayari kwa mechi ambayo imepigwa dhidi ya Leicester City wikendi iliyopita. 

No comments