KING MALUU AENDELEA KUSISITIZA MSIMAMO WAKE WA KUTOREJEA KWENYE MUZIKI WA DANSI

KING Maluu ambaye ni mpulizaji gwiji wa Domo la Bata amesisitiza kuwa kuliko kurejea kwenye majukwaa ya bendi za dansi Bongo, ni afadhali amfundishe mke wake Mwanaali Kinabo kuimba kasha waanzishe kundi lao la watu wachache.

Maluu aliachana rasmi na masuala ya muziki mwaka 1990 na kupiga marufuku watoto wake wote watano kujiingiza kwenye fani ya dansi, baada ya kuona hali ya sanaa hiyo imeanza kuwa ngumu hususan katika kipato.


“Ninachoshukuru mke wangu ana “aidia” ya uimbaji na zaidi ya hilo uimbaji wa siku hizi hauna kazi sana kama kipindi kile (enzi zao), hivyo nitamfundisha taratibu ili akishakuwa sawa tutaanzisha bendi yetu kama ilivyo kwa Abdul Salvador na wengineo,” amesema.

No comments