KING MALUU AWACHANA WANAMUZIKI WA ZAMANI... asema walipata pesa ila walijisahau na kushindwa kujenga maisha

MKONGWE wa Domo la Bata, King Maluu amefafanua kuwa muziki wa zamani ulikuwa unalipa tofauti na madai ya wengi kwamba haukuwa na maslahi na kufanya wasanii wengi waishie kwenye umasikini pamoja na umaarufu wao.


Akiongea jana kwenye kipindi cha Afro Tz cha Radio One Stereo chini ya mtangazaji Rajab Zomboko, Maluu alisema kwamba kilichowaponza wasanii wengi ni kule kudhani kwamba wangeendelea kupata pesa milele yote na hivyo kujisahau katika kupanga maisha yao ya baadae.

No comments