KING MALUU ROHO NYEUPEE KWA BARNABA CLASIC... asema anamchukulia kama mtoto wake wa kumzaa

INGAWA ameshafanya kazi na wasanii wengi wa bongofleva hapa Bongo, lakini mkongwe wa Saxophone, King Maluu anasema kwa upande wake, Barnaba Elias “Barnaba Classic” ndie pekee aliyemweka rohoni na kumchukulia kaka mtoto wake wa kumzaa.

“Hunambii kitu na Barnaba, kwa sababu kwa upande wangu namuona ni msanii anayejitambua zaidi na kujali utu wa kila mtu bila kujali matabaka,” amesema maluu.

Miongoni mwa matukio yaliyompandisha chati Barnaba mbele ya King Maluu ni lile la kumsaidia fedha taslim shilingi laki mbili mara tu alipopata taarifa kuwa mkongwe huyo amekatika kidole na mnyororo wa pikipiki yake wakati akiisafisha.
“Tofauti na wasanii wengine wa bongofleva ambao niliwatumia meseji za simu na kuonekana kutoshituka, Barnaba aliona tu kupitia mitandao lakini akanipigia simu haraka na kunitaka nifike nyumbani kwake akanipe pole,” amesema.

No comments