Habari

KIPUTE CHA SIMBA SC, MBAO FC CHASOGEZWA MBELE… sasa ni hadi Aprili 10 badala ya 8

on

MCHEZO wa
Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara kati ya wenyeji Mbao FC na Smba FC ya Dar es
Salaam uliokuwa ufanyike Aprili 8, mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza
umesogezwa mbele kwa siku mbili hadi Aprili, 10.
Taarifa ya
Mkurugenzi wa Bodi ya ligi, Boniphace Wambura (pichani)imesema kwamba hatua
hiyo imechukuliwa ili kupisha shughuli za kijamii kwenye uwanja huo
zitakazoanza Aprili 1 hadi 9.
Simba SC
inatarajiwa kuondoka Dar es salaam katikati ya wiki kwenda mikoa ya kanda ya
Ziwa kwa mechi zake za Ligi kuu, Ikianzia Bukoba itakapomenyana na Kagera Sugar
Aprili 2, na baadaye mbao FC Aprili 10 na kumalizia na Toto Africans Aprili 15.
Ikumbukwe Simba
SC ndiyo inaongoza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa pointi zake 55
ikifuatiwa na mabingwa watetezi,Yanga SC wenye pointi 53 baada ya timu zote
kucheza mechi 24.

Wakati Simba
SC wakienda kucheza mechi za mwisho za ugenini mikoani, mahasimu wao Yanga
watakuwa na michezo mfululizo ya nyumbani kuanzia Aprili1 na Azam FC,Uwanja wa
Taifa, Dar es salaam.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *