KLOPP ASHAURIWA KUMNG'OA JERMAIN DEFOE SUNDERLAND
KUPEPESUKA kwa Liverpool msimu huu licha ya kuanza na makali kumetokana na kukosekana na watu wanaojituma wakati wote.

Na sasa kocha mkuu wa klabu hiyo, Jurgen Klopp ameambiwa kwamba kama anataka kuiona Liverpool inanyakua ubingwa anatakiwa kubadili mitazamo yake.

Nyota wa zamani wa klabu hiyo, Ronnie Whelan amesema kwamba anadhani kocha huyo anataki kumsajili nyota wa klabu ya Sunderland, Jermain Defoe.

Nyota huyo wa zamani raia wa Jamhuri ya Ireland ambaye alikuwa akipachika mabao anavyotaka wakati akiwa na wekundu hao, amesema kwamba Defoe pamoja na umri wake anawseza kuwa mkombozi wa safu ya ushambuliaji ya Liverpool.
 
“Defoe ana umri ambao nadhani unafika miaka 34 sasa, lakini ukiniuliza ni aina gani ya straika anaweza kuwa nyota pale Liverpool nakwambia simuoni mwingine zaidi yake.
Amesema.

No comments