KOCHA ANTONIO CONTE AMKINGIA KIFUA DIEGO COSTA... asema anamuonyesha tabia nzuri, ni mpambanaji wa timu

LICHA ya mwishoni mwa wiki straika Diego Costa kukwaruzana na baadhi ya wachezaji wa Stoke City, kocha wake Antonio Conte amemkingia kifua akisema kuwa alionyesha nidhamu ya hali ya juu katika mchezo huo wa Ligi Kuu England ambao waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Katika mchezo huo straika huyo mtata alianza vurugu na mabeki wa Stoke City, baada ya kufanyiwa madhambi na alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 17 wakati alipopandisha hasira, baada ya kuanguka kirahisi wakati alipoguswa na nyota wa Stoke City, Bruno Martins Indi.

Mbali na tukio hilo alikwaruzana na wachezaji, Ryan Shawcross na Phill Bardsley wakati mchezo ukiendelea, lakini hata hivyo Conte anapongeza nidhamu iliyoonyeshwa na mchezaji wake kwa kujizuia ili asilimwe kadi nyekundu.

“Nadhani Diego amecheza vizuri na ameonyesha nidhamu ya hali ya juu kwa sababu sio rahisi kwa kuanza mechi kwa ukapewa kadi ya njano na ukamaliza mchezo,” alisema Conte katika mahojiano na wahandishi wa habari mara baada ya mechi hiyo.


Diego amenionyesha tabia nzuri, ni mpambanaji wa timu. Nataka aendelee hivyo na nadhani ni mchezaji mzuri mno,” aliongeza Muitaliano huyo.

No comments