KOCHA DOTMUND AKATA TAMAA YA UBINGWA WA BUNDESLIGA

KOCHA wa Borussia Dortmund, Thomas Tuchel ameonyesha kukata tamaa ya kutwaa ubingwa ndani ya Bundesliga na kusema anapambana kwa ajili ya kuhakikisha timu inacheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Akinukuliwa, Tuchel alisema tofauti na msimu ulipoanza ambapo alikuwa na matumaini makubwa kwa vijana wake, lakini sasa ndoto ya kutwaa ubingwa ni kama imepotea.

“Tulianza msimu vizuri, kila mchezaji alikuwa na ari na hamasa ya kupambana kwa ajili ya ubingwa wa Ujerumani.”

“Hatutofanya makosa ya miaka miwili iliyopita. Hatukuwa katika kiwango bora cha ushindani tofauti na mwaka huu.”

“Tulipambana kuanzia mwanzo, lakini kadri Ligi inavyoendelea nadhani hatuna nafasi ya kuwa mabingwa bali hivi sasa tunapambana ili kupata nafasi ya kucheza michuano ya Ligi ya Ulaya,” alisema Tuchel.

Timu ya Dortmund msimu huu ilionyesha kuyumba baada ya kuwakosa baadhi ya nyota wake waliohamia timu mbalimbali barani Ulaya wakiwemo beki Mats Hummels, Ilkay Gundogan na Henrikh Mkhitaryan.


Lakini kocha Tuchel aliamini ana kikosi cha kupambana kwa ajili ya ubingwa, hata hivyo ndoto hizo zimeyeyuka huku akiamini kuwa Bayern Munich watatetea tena taji la uchampioni wa Bundesliga msimu huu.

No comments