KOCHA JOSE MOURINHO ARUSHA KIJEMBE KINGINE KWA ANTONIO CONTE

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho ni kama kumrushia tena kijembe mwenzake wa Chelsea, Antonio Conte, baada ya kusema kuwa anashangazwa na uchezaji wa timu hiyo ikiwa chini ya Muitariano huyo.

Katika kipindi ambacho aliiongoza mara mbili Chelsea, Mreno huyo alikuwa akishutumiwa kwa mfumo wake wa kupaki basi, lakini juzi katika mahojiano na kipindi cha michezo cha BBC Football Focus, aliludia tena kejeli zake alizozitoa mwezi uliopita akidai kuwa mafanikio  ya Conte kuongoza katika mbio za kuwania ubingwa yanatokana na kwamba timu hiyo inacheza mchezo wa kujihami.

“Hapana, sishangazwi na mafanikio ya Cheasea msimu huu. Kinachonishangaza ni kwa jinsi wanavyocheza,” alisema Mourinho ambaye timu yake ya Man United msimu huu imefunga mabao 39 ikilinganishwa na Cheasea yenye 57.

Alisema kuwa anashangaa sana kwa sababu wanavyodhani wanalazimisha kucheza aina tofauti ya mchezo.


Alisema kwamba licha yakuwa anafahamu Cheasea ni wazuri lakini wanashangaza kwa kucheza soka lakujihami.

No comments