Habari

KOCHA LUIS ENRIQUE YAMEMFIKA HAPA! AAMUA ‘KUBWAGA’ MANYANGA BARCELONA

on

Luis Enrique ametangaza kuwa hataifundisha Barcelona msimu ujao na tayari kocha wa Everton Ronald Koeman anatajwa kuwa mmoja wa watu watakaowania nafasi ya kumrithi Enrique.
Kocha huyo mwenye wa miaka 46 alisema katika mkutano wa waandishi wa habari: “Nitamaliza mkutano huu kwa staili tofauti. Nataka kutangaza kuwa sitaifundisha Barcelona msimu ujao.
“Nataka kuishukuru Barcelona kwa uaminifu waliouonyesha kwangu. Hii imekuwa ni miaka mitatu itakayoacha kumbukumbu isiyofutika.
“Hupati muda wa kupumzika katika kazi hii na sasa nahitaji kupumzika. Natumai tumebakika miezi mitatu yenye changamoto kubwa na bado tuna nafasi kushinda Champions League kama si La Liga”.
Luis Enrique alichaguliwa kuwa kocha wa Barcelona Julai 2014 na hadi sasa ameiongoza klabu hiyo katika mechi 164 akishinda mara 125, sare 81 na kupoteza 18.
Ameipa Barcelona mataji ya  La Liga (2015, 2016), Copa del Rey (2015, 2016), Spanish Super Cup (2016), Champions League (2015), UEFA Super Cup (2015) na  FIFA World Club Cup (2015).
Hivi karibuni kocha huyo amekuwa akishutumiwa kwa mwendo usiotabirika wa klabu yake, hatua ambayo inaweza kuwa imechangia kumfanya aghairi mpango wa kusaini mkataba mpya.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *