KOCHA WA AFRICAN LYON ATOA ONYO KWA WAAMUZI MECHI ZA MWISHO LIGI KUU BARA

KOCHA wa timu ya African Lyon ya jijini Dar es Salaam, Ernest Otieno raia wa Uganda, amewataka waamuzi wanaochezesha Ligi Kuu kuwa makini katika mechi za mwisho.

Akiongea na Saluti5, kocha huyo alisema ikiwa waamuzi watachezesha kihalali ana uhakika timu yake itabakia Ligi Kuu.

Otieno alisema kuwa licha ya timu yake kutofanya vyema sana kutokana na kutatizwa na uzoefu, anaamini wanaweza kupambana kuepuka janga la kushuka daraja.


“Timu yetu haiku sehemu salama, lakini nadhani kama waamuzi watachezesha kwa haki tutafanya vizuri na kuepuka kushuka daraja,” alisema.

No comments