KOCHA WA UFARANSA DIDIER DESCHAMPS ASEMA POBGA NI BONGE LA MCHEZAJI


Kocha wa Ufaransa Didier Deschamps ameungana na kocha wa Manchester United Jose Mourinho kumtetea kiungo anayeandamwa sana Paul Pobga.

Wachambuzi wa soka wamekuwa wakihoji uwezo wa Pobga huku wengi wao wakisema hafanani na thamani yake ya pauni milioni 89.

Lakini Mourinho akiongea kwenye mkutano wa waandishi wa habari siku ya Jumatano, akasema hayumbishwi na wachambuzi juu ya imani yake kwa Pobga.

Na sasa kocha wa Ufaransa Didier Deschamps nae ameibuka na kusema Pobga ni bonge la mchezaji na yuko katika kiwango bora.

Deschamps amesema: “Nadhani anacheza vizuri kwa klabu yake ingawa bado hajaweza kutatua matatizo yote waliyokuwa nayo United.

“Watu wanazungumza sana kuhusu Paul, lakini napenda kile anachofanya kwa United na kwa Ufaransa”.

No comments