LIGI YA SOKA LA WANAWAKE BONGO YAANZA RASMI VIWANJA VYA KARUME DAR

KINYANG’ANYIRO cha Ligi Kuu ya soka ya wanawake nchini hatua ya 6 Bora imeanza rasmi Jumapili hii.

Kwa mujibu wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Ligi hiyo inachezwa kwenye kituo kimoja cha uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Timu sita zilizojikatia tiketi ya hatua ya 6 Bora ni JKT Queens ya Dar es Salaam, Mlandizi Queens ya Pwani na Fair Play ya Tanga kutoka Kundi “A”, wakati kutoka Kundi “B” zimo Marsh Academy ya Mwanza, Sisterz ya Kigoma na Panama ya Iringa.


Ligi hiyo ndiyo itakayomtoa bingwa wa soka la wanawake nchini, ikiwa ni mara ya kwanza kuchezwa kwa Ligi Kuu ya wanawake ingawa upatikanaji wa timu uligubikwa na utata.

No comments