LIVERPOOL, TOTTEN HAM ZAPIGANA VIKUMBO KUWANIA SAINI YA LUCAS ALARIO WA RIVER PLATE

LIVERPOOL ya Jurgen Klopp imeingia katika kupigana vikumbo na Totten Ham na kujikuta wote wakiwania saini ya mfumania nyavu wa timu ya River Plate, Lucas Alario.

Alario yuko katika kiwango cha juu cha soka kiasi cha kuziingiza vitani klabu hizo vigogo wa Ligi ya primier.

Straika huyo mwenye umri wa miaka 23, ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya wakubwa ya nchini kwa Argentina.

Hatua ya kuitwa kwake kucheza sambamba na Lionel Messi kumempa heshima ya hali ya juu ya kisoka na sasa anawindwa na timu zikiwemo Liverpool na Spurs.

Liverpool wameweka mezani ofa ya pauni mil 12, ingawa klabu ya River Plate imebainisha dau la kuuzwa kwa Alario ni pauni mil 15.2.

Kwa mujibu wa jarida la The Sun limeweka bayana azma ya kocha Jurgen Klopp kuvutiwa na straika huyo.

Lakini hata hivyo, ameweka mezani ofa ya pauni mil 8.5, fedha ambayo River Plate wanazikataa.


Pamoja na Liverpool na Spurs, pia timu za Inter Milan na Torino za nchini Italia zimo katika mawindo ya saini ya Alario.

No comments