LIVERPOOL WAINGIA VITANI KUWANIA SAINI YA LUCAS VAZQUEZ WA REAL MADRID

MAJOGOO wa jiji la London wanapigana vikumbo na baadhi ya klabu zinazomfukuzia nyota wa Real Madrid, Lucas Vazquez.

Lakini wanalazimika kuweka dau la ziada mezani la pauni mil 24 kwa ajili ya jembe hilo.

Lucas amekuwa akihusishwa na kujiunga na Liverpool katika usajili ujao wa dirisha la kiangazi.

Lakini Liverpool inawabidi kupambana kwa ajili ya winga huyo wa kulia ambaye pia anawaniwa kwa karibu na Manchester United.

United wanatajwa katika dili la kumfukuzia nyota huyo wa Real Madrid kwa ajili ya kuimarisha kikosi cha mashetani wekundu hao kwa ajili ya msimu ujao.

Lakini taarifa zinasema, tayari kocha Jurgen Klopp ameanza mazungumzo ya awali na raia huyo wa Hispania kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake kinachopambana kuirejeshea klabu hadhi yake ya awali.


Awali Liverpool waliweka mezani dau la pauni mil 15 kwa ajili ya Lucas, lakini klabu ya Real Madrid haijaweka bayana kama wanataka kumuuza winga huyo, licha ya kutokuwa na namba ya kudumu kikosini.

No comments