LUIS ENRIQUE AONDOA MATUMAINI YA USHINDI KWA BARCA DHIDI YA PSG LIGI YA MABINGWA

KOCHA Luis Enrique ni kama amepotezea matumaini kabla ya Barcelona kuivaa Paris Saint-Germain katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kusema kuwa itakuwa miujiza kwao kushinda.

Juzi Barca Walipata ushindi mnono dhidi ya CeltaVigo wa mabao 5-0 katika michuano ya La Liga, ikiwa ni baada ya katikati ya wiki kutembeza kipigo cha mabao 6-1 dhidi ya Sporting Gijon, jambo ambalo liliwafanya kwenda kuivaa PSG wakiwa katika hali nzuri.

Hata hivyo, vijana wa Unai Emery watakwenda kuivaa Barca wakiwa na faida ya mabao 4-0 waliyoyapata wakiwa nyumbani kwao jijini Paris na sasa Luis Enrique anasema kuwa hana matumaini kuwa vinara hao wa Catalans wataweza kusonga mbele.

“PSG watatushambulia na wala hawatajihami kama ilivyokuwa kwa Celta,” kocha huyo aliliambia jarida la Movistar Partidazo.

“Lakini imani yetu ndio msingi,” aliongeza kocha huyo.

Ushindi huo wa Jumamosi ulikuwa ni wa kwanza tangu Luis Enrique alipotangaza mpango wa kung’atuka mwishoni mwa msimu huu na sasa Barca inaonekana kuonyesha kile ambacho kinaungwa mkono na mashabiki.

No comments