MAJERUHI YAANZA KUITESA MANCHESTER UNITED… wachezaji saba huenda wakakosekana dhidi ya West Brom

HALI si nzuri ndani ya Manchester United kutokana na majeruhi yanayokiandama kikosi hicho kinachotafuta nafasi nne za juu katika Ligi Kuu ya England.

Lakini mbio hizo zinaweza kuingia doa kwa vile hadi sasa wachezaji saba wa kikosi hicho wanaweza kutokuwepo katika mchezo wao wa Ligi mwishoni mwa wiki dhidi ya West Brom.

Hali hiyo inaweza kumpa mtihani kocha Jose Mourinho wa juu ya nani aanze katika kikosi cha kwanza.

Zlatan Ibrahimovic atakuwa anamaliza adhabu yake ya kadi nyekundu huku Andre Herrera nae akitumikia adhabu.

Phil Jones aliumizwa na Cris Smalling katika mazoezi ya timu ya taifa, huku Smailling nae akiumia wakati akiwa na timu ya taifa.

Kiungo wa timu hiyo, Paul Pogba nae bado anauguza majeraha aliyoyapata kabla hata ya mechi za mataifa kuanza.

Kiungo Marouane Fellaini nae bado ni majeruhi huku Wayne Rooney akiendelea kupona maumivu ya kifundo cha mguu ambayo yalimfanya atoswe katika kikosi cha timu ya taifa ya England.

Kutokana na matatizo ya kuumia kwa wachezaji muhimu, yanaifanya United kuonekana kama wana kikosi finyu, hali iliyopelekea matajiri wa United kutaka kuongeza majina makubwa mwishoni mwa msimu. 


Tayari United wanasemekana kumalizana mazungumzo ya awali na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid, lakini pia kukiibuka tetesi mpya kwamba miamba hiyo wanamtaka kwa nguvu zote nyota wa Barcelona na timu ya taifa ya Brazil, Neymar.

No comments