MAKUBWA HAYA... ETI ANTONIO VALENCIA ANAJIONA KAMA KINDA WA MIAKA 21!

BEKI wa Manchester United, Antonio Valencia amesema kwamba anajihisi kama kinda wa miaka 21 kutokana na kwamba haoni dalili za kushindwa kung’ara akiwa na klabu hiyo ya Old Traflod.

Akiwa na umri wa miaka 31, Valencia ni mmoja kati ya wachezaji wakonwe Man United, lakini staa huyo raia wa Ecuador pamoja na umri huo anaonekana kuwa tegemeo kiasi cha kuaminiwa mno na kocha wake, Jose Mournho kama beki bora wa kulia katika michuano ya Ligi Kuu England.

Hadi sasa msimu huu, Valencea ameshashuka dimbani mara 33 katika mashindano yote iliyocheza Man United na ana mpango wa kuendelea kuitumikia hata baada ya mkataba wake kumalizika mwakani.

“Tangu awali nimeshabadilisha kila, lakini malengo yangu ni kujituma zaidi mazoezini na kiu yangu ni kuendelea kuimarika zaidi na ndoto zangu ni kuendelea kubaki hapa Man United, na najihisi kama bado nina miaka 21,” Valencea aliiambia tovuti ya Man United.


“Naishukuru taasisi hii ambayo ina klabu ambayo ilinipa nafasi ya kutimiza ndoto zangu, hivyo basi nitaendelea kupambana vikali ili niweze kuendelea kubaki mahali hapa kwa muda mrefu,” aliongea.

No comments