MANCHESTER CITY SASA YAMNYEMELEA LUKASZ PISZCZEK WA BORUSSIA DORTMUND

BOSI wa matajiri wa jiji la Manchester, Manchester City, Pep Guardiola ameamua kugeukia wachezaji wa Bundesliga na sasa anamwinda nyota wa Borussia Dortmund, Lukasz Piszczek.

City imekuwa katika mbio za kumsainisha nyota huyo kwa dau la pauni mil 35.

Hatua ya city kutaka kumwita kundini mlinzi huyo ni kutokana na mkakati wake wa kutaka kusuka kikosi imara cha kuipa mataji klabu.


Akinukuliwa, Pep alisema: “Lukasz Piszczek ni kati ya wachezaji muhimu kwa sasa walio katika kiwango cha juu, ana kipaji cha kuweza kucheza katika klabu yoyote kubwa hivyo City haipaswi kumwacha.”

No comments