MANCHESTER CITY YATOZWA FAINI YA PAUNI 35,000 KWA WACHEZAJI KUONYESHA UTOVU WA NIDHAMU UWANJANI

KLABU ya Manchester City imetozwa faini ya pauni 35,000 kufuatia kulalamika mbele ya mwamuzi wakati alipotoa adhabu ya penati kwenye mchezo dhidi ya Liverpool.

Man City wamepewa onyo kwa kushindwa kuwazuia wachezaji wao kuwa na nidhamu uwanjani kiasi cha kumzonga mwamuzi kila wakati.

Hali hiyo inafuatia tukio la dakika ya 50 baada ya mwamuzi Michael Oliver kuizawadia Liverpool mkwaju wa penati.
James Milner aliandika bao kwa mkwaju huo huku Sergio Aguero akisawazisha katika dakika ya 69.


Katika mchezo huo ulioisha kwa sare ya 1-1, gaer Clichy alimchezea vibaya mshambuliaji Roberto Firmino wa Liverpool na kusababisha penati hiyo.

No comments