MANCHESTER UNITED YAPATA 'AHUENI' ROBO FAINALI YA EUROPA LEAGUE


Manchester United imepata ratiba yenye ahueni katika robo fainali za Europa League ambapo itamenyana na Anderlecht  ya Ubelgiji.

Kikosi cha Jose Mourinho kilichoitoa Rostov ya Urusi, kimebahatika kupangiwa safari fupi ya kwenda mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels.

Mechi zote za robo fainali ya Europa League zitakazochezwa April 13 na kurudiwa April 20, ni:
Anderlecht vs Manchester United
Celta Vigo vs Genk
Ajax vs Schalke
Lyon vs Besiktas 
No comments