MARUFUKU YA GUARDIOLA KWENYE “CHOCOLATE” YAWASHANGAZA WACHEZAJI MANCHESTER CITY

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola ni kama amewakwaza wachezaji wake kutokana na mbinu mpya ambazo amekuja nazo katika soka.

Kocha huyo raia wa Hispania amewazuia wachezaji wake kula baadhi ya vyakula vikiwemo vile ambavyo wamekuwa wakivipenda zaidi.

Juzi kocha huyo ameonekana kuwashangaza wachezaji wake baada ya kuamua kupiga marufuku kuuzwa kwa bidhaa aina ya chocolate kwenye viwanja vya mazoezi vya Manchester City na kwenye timu za vijana.

Uamuazi huu umeonekana kuwashangaza baadhi ya wachezaji wanaopenda kutumia bidhaa hizo na sasa wanalazimika kuzitumia kwa siri kana kwamba zimekuwa bidhaa haramu.

Hata hivyo chocolate zilizonunuliwa kwingine bado zinaruhusiwa maeneo hayo, hivyo wafanyakazi watatakiwa kujipanga ili kupata vyakula hivyo kama watahitaji kula.


Lakini pia mashabiki wawe na amani kwani chocolate itapatikana uwanjani kwa ajili ya mashabiki siku za mechi tofauti.

No comments