MASHABIKI WA LEICESTER CITY "WAMKATAA" KOCHA ROY HODGSON

MASHABIKI wa klabu ya Leicester City ya Uingereza wameanza kuonyesha wasiwasi wao katika jitihada za kusaka kocha ambaye anatarajiwa kutwaa mikoba ya Claudio Ranieri.

Wakiwa wamefurika nje ya uwanja wa Kings Power, mashabiki hao wameandika kwenye mabango kwamba kocha anayepewa nafasi ya kwanza katika mazungumzo ndie atakuwa msaada wa kuwaondoa katika tope la kukosaa mafanikio msimu huu.

Kocha anayetajwa sana ni Roy Hodgson ambaye hajawahi kuwa na mafanikio makubwa katika timu ambazo amefundisha ikiwemo Liverpool FC.

Mashabiki hao wamesema kwamba hawaoni kama viongozi wao wako siriazi katika kusaka mbadala wa Ranieri kwani wanaona kuwa ni kama anakuja kocha ambaye amezidiwa kila kitu na kocha aliyefukuzwa.


Kocha huyo wa zamani wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson anatajwa kama kocha anayefikiriwa kupewa mikoba iliyoachwa na Ranieri ndani ya Leicester City ambayo kwa sasa ipo chini ya kocha msaidizi wa Ranieri, Craig Shakespeare.

No comments