MASHABIKI WAVURUGA PAMBANO LA SENEGAL, IVORY COAST UFARANSA

MASHABIKI wamevuruga mechi ya kirafiki kati ya Senegal na Ivory Coast iliyokuwa ikipigwa jijini Paris, Ufaransa.
Mechi hiyo ilisimamishwa wakati mashabiki walipoingia uwanjani na kuleta tafrani.

Miamba hiyo ya Afrika ilikuwa sare ya goli 1-1 katika dakika ya 88 wakati mashabiki wachache walipoingia uwanjani, huku mmoja akionekana kumrukia mchezaji wa Senegar, Lamine Gassama.

Wachezaji walitoka uwanjani na mwamuzi Tony Chapron akaamua kuisimamisha mechi hiyo.

Mshambuliaji wa Liverpool, Sadio Mane alikuwa ameipa Senegal goli la kuongoza mnamo kipindi cha pili, lakini Zoro Cyriac Gohobi akasawazisha dakika tatu baadae.

Mwandishi wa habari wa shirika la L’Equipe Herve aliyekuwepo uwanjani wakati huo aliiambia BBC Sports kuwa tukio hilo lingekuwa baya.

“Sitoweza kusema kuwa watu walikuwa na ghasia lakini ni kama walikuwa wanajaribu kuwafikia wachezaji,” mwandishi huyo alieleza.


Hiyo ilikuwa ni mara ya pili ndani ya miaka mitano mechi kati ya nchi hizo kusimamishwa kutokana na vurugu za mashabiki.

No comments