Mashauzi Classic chini ya Isha Mashauzi leo usiku (Jumatano hii) watakuwa na show kubwa ndani ya club ya kimataifa Next Door Masaki huku mastaa kibao wa kike wakitarajiwa kupamba onyesho hilo.

Show hiyo ni maalum kwa kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani inayofanyika Machi 8 kila mwaka na moja ya zawadi kubwa kutoka kwa Isha Mashauzi ni wimbo wake mpya kabisa “Mwanamke Mpango Mzima” ulioachiwa hewani wiki iliyopita.

Kama vile hiyo haitoshi, show hiyo pia itakuwa ni sehemu ya kusherehekea miaka mitano ya kipindi cha Ng’ari Ng’ari cha Clouds TV.

Baadhi ya watangazaji maarufu wa vipindi vya muziki wa mwambao nao wanatarajiwa kutinga Next Door.

USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac