MASHAUZI CLASSIC WAJA NA USIKU WA THAMANI YA MAMA ALHAMISI HII MANGO GARDEN


Mashauzi Classic chini yake Isha Mashauzi “Queen of the Best Melodies”, Alhamisi hii wanakuja na kitu matata ndani ya ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Kitu hicho matata si kingine bali ni usiku maalum wa “Thamani ya Mama” ambao utatoa fursa kwa watu kuonyesha upendo mubashara kwa mama zao – iwe mama mzazi, mama mdogo, mama mlezi, mama mkwe au hata mama wa kambo.

Usiku huo wa Thamani ya Mama utasindikizwa na burudani ya kukata na shoka kutoka kwa kundi zima la Mashauzi Classic huku wakisindikizwa na Kibao Kata Ng’aring’ari.

Isha Mashauzi ameiambia Saluti5 kuwa siku hiyo ataimba nyimbo zake zote zinazomzunguzia mama au mwanamke.

Amezitaja nyimbo hizo kuwa ni “Mama Nipe Radhi”, Nani Kama Mama”, “Mwanamke Mpango Mzima” pamoja na ule mpya kabisa ambao bado haujarekodiwa uliopewa jina la “Thamani ya Mama”.

Mkurugenzi huyo wa Mashauzi Classic akafafanua kuwa onyesho hilo ni mwendelezo wa kanuni zao za kufanya onyesho kubwa ndani ya Mango Garden kila Alhamisi ya mwisho wa mwezi.

No comments