Habari

MASKINI ARSENAL!!! ALEXIS SANCHEZ APASUA JIPU PWAAA

on

ALEXIS SANCHEZ ameendelea kuwachanganya Arsenal baada kutoa kauli tata kuwa anataka kuchezea timu ya ushindi.
Mshambuliaji huyo wa Chile amesema anataka kubaki katika jiji la London kwa timu itakayopigania mataji, hiyo ikimaanisha kuwa yuko njia panda kubaki Arsenal.
Kauli hiyo imetafsiriwa kuwa safari ya kujiunga na Chelsea imepamba moto, kwani hiyo ndo klabu pekee ya London yenye rekodi nzuri ya kutwaa mataji katika miaka ya karibuni.
Katika habari iliyochapishwa na Metro la Uingereza, Sanchez amenukuliwa akisema: “Nina furaha London na nategemea kumaliza mkataba wangu Arsenal.
“Nataka kukaa kwenye timu ya ushindi, timu yenye utashi wa kupigania mataji. Nina umri wa miaka 28, bado kuna mengi mbele yangu.”

Comments

comments

About Saluti 5

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *