MASTAA WAKESHA KWENYE MITANDAO USHINDI WA BARCELONA DHIDI YA PSG

ACHANA na ushindi mkubwa wa ajabu wa mabao 6-1 ambao FC Barcelona umeupata dhidi ya PSG ya Ufaransa.

Ndani ya ushindi huo kuna mambo kadhaa yasiyo ya kawaida yamefanyika na sasa yamekuwa gumzo mitandaoni.

Baada ya goli la sita la Sergio Roberto dhidi ya PSG, mitandao ilikuwa bize, hasa Twitter.

Dakika saba baada ya goli hilo, kila timu ilikuwa ikitweet kuhusu goli hilo, Sergio Robert aliufanya mtandao kuwa bize sana na kila mtu alisema lake kuhusiana na bao hilo.

Inadaiwa kuwa baadae mtandao huo ulikuwa kama umezidiwa kutokana na jinsi watu walivyokuwa wakitupia meseji akiwemo nyota wa zamani wa kikosi hicho, Thierry Henry.

Mshambuliaji huyo wa kiwango cha juu kuwahi kutokea, aliandika neno moja tu “waaoh!” kiasi cha kuonyesha kwamba furaha yake ilimkausha maneno.

Nae kiungo wa Everton, Ross Barkley aliyekuwa akiangalia mchezo huo kupitia televicheni, nae akakiri kuwa ameshuhudia tukio hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter. 
  
Barkley aliandika: “Nilichokishuhudia ni moto.” Hapa kwa kauli yake mubashara alikiri kwamba mziki wa Barcelona ulikuwa moto.

Nae beki wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdnando alikiri hiyo ni miujiza mikali kuwahi kuona katika maisha yake ya soka.

“Sijawahi kuona timu ikibadilisha matendo kama leo,” aliandika Ferdinando katika ukurasa wake wa Twitter.

Nae Joey Barton, kiungo mkorofi pia hakuwa nyuma kwani kupitia ukurasa wake aliandika: “Sijawahi kuona kitu kama hiki.”

Rory Smith ni mmoja kati ya wachezaji maarufu nchini Canada, yeye aliandika tu “Mungu wangu” akionekana kushangazwa na kilichotokea.

Nyota mwingine wa michezo, Tim Peach ambaye ni mwigizaji maarufu nchini Uingereza na Ujerumani, yeye alienda mbali zaidi kwa kuutumia mchezo huo kuwatania Arsenal.


Peach ameandika: “Leo ndio nimejua kuwa kwanini Wenger anafaa kuwa kocha wa PSG.” Hiyo inatokana na Wenger nae kupata kipigo kikubwa kutoka kwa Bayern Munich.

No comments