MATS HUMMELS AKANUSHA KUHUSISHWA KUONDOKA BAYERN MUNICH… asema bado yupoyupo sana tu Bundesliga

MLINZI wa timu ya Bayern Munich, Mats Hummels amezisikia taarifa za kutaka kuondoka na sasa amekanusha akisema bado yupoyupo kwanza Bundesliga.

Hummels anayeitumikia pia timu ya taifa ya Ujerumani, mkataba wake unafika tamati majira ya mwaka 2021 ndani ya kikosi cha mabingwa hao watetezi.

Hatua hiyo inazifanya klabu mbalimbali za Ulaya kutaka kupata saini yake na klabu za Arsenal, Real Madrid na Manchester United kugonga mwamba.

Mlinzi huyo aliyeng’ara katika fainali za Kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil, amesema kuwa kwa sasa anataka kutuliza akili zake akiwa na Munich.

“Uvumi wote huo ni jambo linguine ambalo sijaliweka katika vipaumbele vyangu, nitaendelea kuvumilia kusikia haya.”
“Ninachoweza kusema ni kwamba ninaamini tuna kikosi kizuri kwa ajili ya misimu yote nikiwa hapa.”

Hummels mwenye umri wa miaka 29, amekuwa kati ya walinzi imara ndani ya Bundesliga.

No comments