MAUA SAMA AFICHUA ALIVYTOPAGAWISHWA NA SIMU YA KWANZA ALIYOPIGIWA NA MWANAFA

MWIMBAJI wa kike wa muziki wa bongofleva, Maua Sama amesema wakati alipokuwa hajulikani kabisa kimuziki alipokea simu kutoka kwa MwanaFA, mtu aliyekuwa akimsikia au kumwona kwenye Tv akimsifia kwa uimbaji wake mahiri.

Ilikuwa ni simu iliyomshitua mwimbaji huyo na akadhani kuwa anataka kuingizwa mjini na wajanja.

“Sikuamini,” Maua alikiambia kipindi cha The Playlist cha radio Times Fm. “Kwanza nilishangaa, si unajua wale watu wa mtandao wanataka kuzingua kwa hiyo kwangu mimi nikaona kabisa nataka kutapeliwa.”

Baada ya FA kujieleza ndipo Maua alipoamini kweli na kuamua kutoroka kupanda basi kuja Dar es Salaam na ndipo wimbo wake wa kwanza “So Crazy” aliomshirikisha FA ulipotoka .

No comments