Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino ameweka wazi kuwa kamwe hawezi kukubali ofa ya kuwa kocha wa Barcelona au Arsenal.

Hivi karibuni kocha huyo alihusishwa na safari ya kujiunga na Barcelona baada ya kuonekana akiwa mazungumzoni na rais wa miamba hiyo ya Hispania Josep Maria Bartomeu.

Hata hivyo Pochettino amesema 'mkutano' huo kati yake na Josep Maria Bartomeu uliotokea tu lakini haukuwa umepangwa na kwamba kamwe hawezi kuwa 'msaliti' kwa klabu yake ya zamani Espanyol yenye upinzani wa jadi na Barcelona.

Pochettino aliitumikia Espanyol kama mchezaji kwa zaidi ya miaka sita kabla ya kuibuka kuwa kocha wa klabu hiyo ikiwa ndio timu yake ya kwanza kuifundisha katika historia ya maisha yake ya ukocha.

Mbali na Barcelona, Pochettino amesema hawezi pia kuifundisha Arsenal kutokana na upinzani uliopo dhidi ya klabu yake ya Tottenham.

 Pochettino enzi hizo akiichezea Espanyol
Pochettino enzi zake za ukocha wa Espanyol

USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac