MBEYA CITY WASEMA MWAMUZI AMEWANUSURU SIMBA NA KIPIGO

KOCHA wa Mbeya City ya jijini Mbeya, Kinna Phiri amesema matokeo ya sare ya 2-2 dhidi ya Simba, sio kitu walichotaka kitokee bali vinara hao wa Ligi walitakiwa kufungwa endapo wasingebebwa na maamuzi yenye utata.

Akiongea na Saluti5, Phiri raia wa Malawi alisema hata kabla ya mchezo huo walijua wazi kwamba wana nafasi kubwa ya kushinda katika mechi hiyo kutokana na kuujua udhaifu wa Simba.

Phiri alisema kuwa, mwamuzi wa mchezo huo alionekana wazi kubabaika na kutoa maamuzi ambayo yalilenga zaidi kuhakikisha Simba haipotezi mechi hiyo licha ya kuzidiwa kila idara.

Alisema, vijana wake walifanikiwa kuwafunika Simba katika mambo mengi uwanjani, lakini maamuzi tata yakawanyima ushindi na hilo wanamuachia Mungu kwa kuwa wanajua hawana jinsi.

Watu walikuja kuangalia mechi ya leo (jana) na wameona tumecheza soka safi, tulistahili kushinda na tulitimiza wajibu wetu kwa kila hali lakini hatukutendewa haki na mwamuzi.”

“Kutoka nao sare ni kutokana na juhudi za waamuzi ambao ni kama walikuja kuhakikisha wanaisaidia Simba isifungwe, kila kitu walichokuwa wanaamua kuhusu sisi hata kama haki ilikuwa yetu walipewa Simba mpaka wakasawazisha.”

No comments