MBEYA CITY WATAMUDU KUMKAZIA MNYAMA MWENYE "HASIRA" ZAKE LEO

TIMU ya Mbeya City “Wagonga Nyundo wa Mbeya” leo Jumamosi wanashuka kwenye dimba la uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam kumenyana na Simba katika mwendelezo wa Ligi.

Swali wanalojiuliza wengi ni je, Mbeya City wataweza kuisimamisha Simba ambayo kwa sasa inaonekana ipo vizuri ikilinganishwa na msimu uliopita?

Mbyea City ilikuwa ni moja ya timu zilizokuwa zikiiwekea ngumu sana Simba katika misimu miwili iliyopita, lakini msimu huu haionekani kuchangamka sana.

Samba kwa sasa ndio wanaoongoza msimamo wa Ligi Kuu wakifuatiwa na Yanga, wakati Mbeya City ambao msimu huu hawajaonyesha cheche zao wapo katikati wakipigania kujiweka katika nafasi salama zaidi ya kubaki Ligi Kuu.


Timu hizo zote zimebakiza mechi saba kila moja kukamilisha msimu huu wa Ligi, hivyo kila moja inapigania kupata matokeo mazuri katika kila mchezo ulio mbele yake. 

No comments