MBEYA CITY YAILIA MAZOEZI MAKALI RUVU SHOOTING

TIMU ya Mbeya City ya jijini Mbeya ni kama inatishia nyau Ruvu Shooting ya Pwani baada ya kudai inaanza mazoezi ya kuiangamiza Jumamosi ijayo.

Mbeya City wamepewa kiburi na sare ya mabao 2-2 waliyoyapata na vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba ya jijini Dar es Salaam, mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam wikiendi iliyopita.

“Mbyea City imeanza mazoezi rasmi kujiandaa kutimuana na Ruvu Shooting ya Mlandizi Pwani kwenye mchezo mwingine wa Ligi hiyo Jumamosi ijayo kwenye uwanja wa Sokoine, mjini hapa,” alisema msemaji wa timu hiyo, Dismas Ten.

Msemaji huyo alisema maandalizi kuelekea mchezo huo yanakwenda vizuri, lengo likiwa ni kuhakikisha si tu inaibuka na ushindi na kujiongezea pointi tatu muhimu, hasa baada ya kuvuna pointi moja uwanja wa Taifa Jumamosi iliyopita mbele ya Simba.


Alisema, mchezo wa Jumamosi dhidi ya Ruvu Shooting ni muhimu kwao na ndio sababu wanafanya maandalizi mapema ili kuhakikisha wanatimiza lengo la kuibuka na ushindi.

No comments