MBEYA CITY YATAMBA KUREJEA KWENYE UBORA WAKE... yatoa tahadhari kwa wapinzani wao katika mechi zijazo

TIMU ya soka ya Mbeya City imejitapa kuwa kuanzia hivi sasa imerudi kwenye njia zake baada ya kuyumba kwa miezi kadhaa.

Akizungumza na Saluti5, msemaji wa timu hiyoDismas Ten alisema kwamba timu hiyo kwa sasa imekaa sawa hivyo wapinzani wao kwenye mechi zijazo wajihadhari.

Alisema kuwa timu hiyo inachokifanya sasa ni kuhakikisha inashinda mechi zijazo na kumaliza Ligi Kuu ikiwa katika nafasi nzuri.


“Timu yetu kwa sasa imeka vizuri, tunawaambia wapinzani wetu kuwa wajiandae, tutahakikisha tunashinda mechi zetu zotezilizosalia katika Ligi Kuu,” alisema.

No comments