MECKY MEXIME ASEMA KAGERA SUGAR ITATISHA LIGI KUU BARA MSIMU UJAO

KOCHA wa timu ya Kagera Sugar, Mecky Mexime amesema kuwa timu hiyo msimu ujao itatisha katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akiongea na Saluti5, Mexime alisema anashukuru kwa hatua waliyofikia mpaka sasa kwani hakutarajia kufanya vyema sana katika msimu huu.

Mexime aliyetua Kagera Sugar akitokea Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani, ameiwezesha Kagera Sugar kurudisha makali yake baada ya kufifia kwa misimu mitatu iliyopita.

“Unapokuwa unaisuka timu upya hutarajii kufanya vizuri, lakini nashukuru kwa hatua tuliyoifikia na naamini msimu ujao tutakuwa kwenye malengo mengine sio kubaki kwenye Ligi Kuu,” alifichua.


Akiwa katika msimu wake wa kwanza, licha ya kuanza Ligi vibaya, Mexime aliiwezesha timu hiyo kupanda hadi nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ingawa wameachwa kwa pointi nyingi na Yanga na Simba zinazochuana kileleni.

No comments