Kwa wale wanaopenda taarab bila chenga, basi onyesho hili la Usiku wa Tashtiti za Pwani, litawafaa sana.

Usiku wa Tashtiti za Pwani utafanyika Jumatatu ijayo Machi 20 ndani ya ukumbi wa Lango la Jiji, Magomeni jijini Dar es Salaam.

Onyesho hilo la aina yake  litapambwa na bendi mbili za taarab East African Melody na Gusa gusa Mind Band ambazo zitaonyeshana ufundi wao.

Kama vile hiyo haitoshi, mwaimbaji mkongwe wa taarab Bi Sabah Salum Muchacho, atakuwa msanii mwaliko kwenye onyesho hilo.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac