MESUT OZIL ASEMA KOCHA PEP GUARDIOLA ALIMZUIA ASIJIUNGE BARCELONA

WAKATI Mesut Ozil akihamia Hispania, Barcelona ilikuwa timu kubwa iliyopewa nafasi ya kumnasa kwa kipindi hicho.

Tofauti na matarajio ya wengi, Ozil aliikacha Barcelona na kujiunga na mahasimu wao wakubwa, Real Madrid.

Mashabiki wengi wa Barcelona walichukizwa sana na kitendo hicho na wengi walimuona Ozil kama ni mtu mwenye tamaa na fedha na ndio maana aliwatosa.

Miaka imekwenda na sasa Ozil hayuko Barcelona wala Madrid, Ozil yuko Arsenal.

Ozil amefichua siri ya kilichotokea miaka kadhaa iliyopita wakati akitoka Werder Bremen ya Ujerumani na kwenda Real Madrid.

Ozil alimtaja Pap Guardiola kwamba ndie mtu ambaye alimfanya asijiunge na Barcelona.

Anadai alimpuuza na hakuwa anataka kuongea nae moja kwa moja kuhusu usajili japokuwa Barcelona ilionyesha nia ya kumtaka.

“Baada ya Kombe la Dunia mwaka 2010, timu niyingi zilinifata na kunihitaji, nakumbuka Barcelona, Bayern Munich, Manchester United, Arsenal, Real Madrid walionyesha nia ya kunihitaji sana.”

“Wakala wangu alikaa na Bayern Munich wakamwambia jinsi gani wananihitaji na wakamweleza malengo yao juu yangu.”
“Baadae wakala wangu akafanya vivyo hivyo na timu nyingine zilizokuwa zikinihitaji,” alisema Ozil.

“Kabla sijaondopka Ujerumani nilianza kushawishika kuwa Barcelona ndiko ambako ningeenda. Walikuwa wakicheza soka linalonivutia sana, ila tatizo linakuja kwa kocha wao naona hakuwa ananitaka mimi kwani hakuwahi kunipigia simu wala kunitumia ujumbe mfupi wa simu, niliona atakuwa haniitaji,” aliongeza Ozil.

Baada ya Ozil kumuona Guardiola kama anamzingua, ndipo aliamua kubadili mawazo na kwenda Madrid ambako nao aliwavutia.

Ozil alijiunga na Madrid kwa ada ya pauni mil 10 na Madrid wakafanikiwa kumuuza kwa faida kubwa ya ada ya pauni mil 42 kwenda Arsenal mwaka 2013.


Kwa sasa mkataba wa Ozil na Arsenal haueleweki na inasemekana Ozil anataka fedha nyingi ili abaki Arsenal nab ado wako kwenye maongezi juu ya mkataba huo.

No comments