MFANYABIASHARA WA CONGO ‘AFIKA BEI’ KWA CHAZ BABA, AMWINGIZA STUDIO ...Elly Chinyama, Mjusi Shemboza nao ndani


Mfanyabishara mkubwa wa Congo - Bismat Junior  ameamua kujikita kwenye uimbaji lakini kwa kufunga safari hadi Tanzania kupata ‘mbeleko’ ya Chaz Baba.

Tajiri huyo mdau mkubwa wa muziki, alituma watu wamtafutie mwimbaji mkali wa dansi la Tanzania na alipotumiwa kazi za Chaz Baba, akafika bei na kuja Bongo kurekodi naye nyimbo iliyopewa jina la “Misha”.

Wimbo huo ambao umeimbwa kwa kiswahili na kilingangala, umerekodiwa juzi katika studio za Classic zilizoko Kigogo jijini Dar es Salaam lakini ‘mastering’ inakwenda kufanywa Congo.

Chaz Baba ambaye amevuta mshiko mrefu kupitia kazi hiyo, akaiambia Saluti5 kuwa kazi imekamilika na kilichobakia ni ‘material’ ya nyimbo hiyo kupelekwa Congo ili kwenda kuongezewa maufundi kabla haijaachiwa hewani.

Wanamuziki walioshiriki kutengeneza wimbo huo ni pamoja na Mjusi Shemboza wa Sikinde aliyepiga gitaa la rhythm na Elly Chinyama aliyekung’uta solo gitaa huku kinanda kikipapaswa na Micky Engineer ambaye pia ndiye aliyekuwa producer.

Bismat Junior akitupia masauti yake
 Bismat Junior akiimba sambamba na Chaz Baba
Elly Chinyama ambaye miezi michache iliyopita alipata ajali mbaya ya kugongwa na pikipiki, alikuwepo studio kupiga solo gitaa
Mjusi Shemboza akipiga gitaa la rhythm 
Chaz Baba akiimba kwa hisia


No comments