MIRALEM PJANIC ATAKA KUSEPA JUVENTUS ILI ATUE MANCHESTER CITY MAJIRA YA KIANGAZI

MIRALEM Pjanic tayari ameonyesha azma ya kutaka kuondoka Juventus ili akatafute maisha mbele ya safari katika usajili huu wa majira ya kiangazi.

Tena amekwenda mbali zaidi kwa kuitaja timu anayoipenda kwenda kukipiga na kwamba mapenzi yake ni kwenda kuvaa uzi wa Manchester City.

Kiungo huyo ameomba uongozi wa klabu ya Juve licha ya kumruhusu aondoke, anataka kwenda kutimiza azma yake ya kucheza Ligi ya premier.

Pjanic ambaye msimu huu amekuwa katika kiwango bora akiwa na Juve, ameweka bayana ndoto yake ya kucheza katika Ligi iliyo na mashabiki wengi.

“Nina malengo ya kutimiza ndoto ya kwenda kucheza katika Ligi ya premier.”

“Ninataka kuona ninalinda kipaji changu, sitaki kuwa msiri juu ya mimi kuondoka hapa.”

“Soka ni kazi ninayokwenda kuifanya popote. Soka ni mchezo wa kuangalia leo na kesho. Huu ndio msimamo wangu kwa sasa,” alisaema Pjanic.


“Manchester City ni klabu ninayoipenda kwa ajili ya soka langu la baadae. Ninaamini nina nafasi ya kucheza nikiwa kule na kutimiza ndoto yangu hii,” aliongeza Pjanic.

No comments