Habari

MOURINHO KUUNDA UKUTA WA ZEGE MAN UNITED KWA KUMSAJILI JOSE GIMENEZ WA ATLETICO MADRID

on

JOSE GIMENEZ  huenda akaondoka  Atletico Madrid kufuatia habari kuwa Jose Mourinho anajipanga kupeleka ofa nono ili kumnyakua sentahafu huyo.
Mourinho yuko sokoni kusaka beki mpya wa kati na anammulika nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay kama mtu sahihi wa kuunda ukuta wa zege Old Trafford.
Kwa mujibu wa Manchester Evening News, Gimenez anavutiwa na safari ya kwenda United baada ya kukosa uhakika wa kuwa chaguo la kwanza kwa kocha Diego Simeone.  
Beki huyo mwenye umri wa miaka 22, ameanza mechi 16 msimu huu wakati Diego Simeone akivutiwa zaidi na pacha ya Diego Godin na Stefan Savic kwenye beki ya kati.
Dau la kuununua mkataba wake ni pauni milioni 56, lakini United inaamini haitalazimika kutoa kitita chote hicho kwa kuwa mkataba huo unafikia ukingoni kiangazi cha 2018, hali inayotishia mchezaji huyo kuondoka bure baada ya msimu ujao.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *