MOUSSA DEMBELE ASEMA KOCHA POCHETINO AMEIBADILI TOTTENHAM KWA KIASI KIKUBWA

STAA Moussa Dembele amesema kwamba anavyoamini kocha wao, Mauricio Pochettino amebadili kila kitu na kuifanya Tottenham kuwa na uhakika wa kutwaa ubingwa.

Dembele alijiungna na Tottenham mwaka 2012 na sasa anasema kuwa anavyoamini Pochettino ameibadili timu katika kipindi cha miaka miwili na nusu iliyopita.

“Nadhani kila timu huwa na malengo ya kushinda mataji ili kujivunia sehemu kubwa ya mafanikio na nadhani sisi tuna kiwango cha kufanya hivyo kwa sasa,” Mbelgiji huyo aliiambia Sky Sports.


“Sio kitu ambacho unaweza kukiangalia kwa kamera, ni aina ya mfumo wa klabu. Kila kitu kwa sasa kimebadilika,” aliongeza kiungo huyo.

No comments