MSONDO NGOMA, SIKINDE NGOMA YA UKAE KUPAMBA UTAMBULISHO WA ORIGINAL DAR MUSICA

BENDI  kongwe za muziki wa dansi, Msondo Ngoma Music Band na Mlimani Park Sikinde zinatarajiwa kupamba utambulisaho wa bendi mpya ya miondoko hiyo, Original Dar Musica, imefahamika.

Bosi wa Original Dar Musica, Jado FFU aliiambia Saluti5 kuwa utambulisho huo umepangwa kufanyika mwezi ujao, ndani ya Mango Gadern, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

“Nimezichagua bendi hizo kupamba shoo yetu ya utambulisho ili kuziupa heshima, kutokana na kwamba ndio bendi kubwa na kongwe zaidi zilizosalia hapa Bongo,” alisema Jado FFU.


Hivi sasa Original Dar Musica wanajiandaa kwa kuingia Studio ya Amoroso Sound wiki ijayo kuachia vibao vyao vitatu ambavyo ni “Hatufanani”, “Jibebishe” na “Mtu Box”.

No comments