MSONDO WAREJESHA TENA ‘MSONDO FAMILY DAY’ … ni siku ya Pasaka ndani ya Bulyaga


HATIMAYE lile onyesho  la Msondo Family Day la mwezi huu kupitia bendi ya Msondo Ngoma Music Band “Baba ya Muziki”  linarejea tena baada ya ukimya wa miezi kadhaa.

Onyesho hilo ambalo lilikuwa likifanyika kila wikiendi ya mwisho wa mwezi, safari hii litarindima ndani ya ukumbi wa New Bulyaga Bar, Temeke jijini Dar es Salaam siku ya Pasaka Aparil 16.

Mmoja wa waratibu wa onyesho hilo, Abdulfareed Hussein, ameimbia Saluti5 kuwa maandalizi ya ujio mpya wa Msondo Family Day tayari yameanza kushika kasi.

Hili litakuwa onyesho la kwanza la Msondo Family Day kwa mwaka huu. Mara ya mwisho lilifanyika Mango Garden Kinondoni Disemba 2 mwaka jana.

Abdulfareed Hussein  amesema kama ilivyo ada, dhumuni la ‘Msondo Family Day’ ni kuongeza mshikamano baina ya wanamuziki wa Msondo, mashabiki na wadau wakubwa wa bendi hiyo ikiwa ni pamoja na kupeana zawadi mbali mbali.

No comments