MWANAMITINDO AFA KWA KUGONGWA NA TRENI WAKATI AKITAFUTA POZI ILI APIGWE PICHA

MWANAMITINDO kinda Fredzania Thompson ameacha majonzi baada ya kufariki dunia akiwa ndio kwanza anaanza kuchanua kwenye ulimwengu wa mitindo.

Mwanamitindo huyo aligongwa na treni na kufa papohapo wakati akitafuta pozi la kupigwa picha.

Fredzania Thompson alikuwa anapigwa picha hizo mpya za mitindo ili zianze kutumika katika kazi zake za mitindo ambazo zilikuwa za kwanza kwake kupigwa kwenye reli.


Polisi wamesema kwamba binti huyo aligongwa na treni wakati akilipisha treni moja bila kujua kwamba kulikuwa na treni jingine likija upande wa pili ambalo lilimgonga na kumuua.

No comments