MWENENDO MBOVU WA JKT RUVU WAWACHUKIZA VIONGOZI MAKAO MAKUU

MWENENDO wa timu ya JKT Ruvu ya Dar es Salaam umewashitua viongozi wa makao makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT Mlalakua).

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mmoja wa viongozi wa timu hiyo ni kuwa, tayari viongozi wa juu wameingiwa na hofu kutokana na matokeo.

Alisema, hawajajua nini kimeikumba timu hiyo ambayo inaundwa na wachezaji wenye uzoefu wa Ligi pamoja na chipukizi wachache.

“Timu hii msimu huu imewakatisha tama viongozi wa juu, maana baada ya kufanya utafiti waliamua kumbadili kocha, walidhani kuwa ndie tatizo lakini imeonekana kuwa tatizo ni wachezaji kwani ujio wa Bakari Shime haujawaondoa mkiani,” alisema.


Alisema, hawana uhakika tena iwapo timu hiyo inayoburuza mkia katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, itazinduka dakika hizi za lala salama na kuepuka kushuka daraja.

No comments